1/11/11

Wazo la Leo

Nchi Gani Ambazo Maskini?


Tofauti kati ya nchi maskini na nchi matajiri si kutokana na historia ya nchi..!!??

Ukitazama Misri na India zina zaidi ya miaka 2000 na ni maskini kuacha nchi zingine za kiafrika na za kiamerika latinia, Ukija kuona kama Canada, Australia na New Zealand zilikuwa hazipo katika miaka 150 iliyopita licha ya kuwa zina maendeleo ya nchi na utajiri.

Japan ina udogo wa asilimia 80% ya eneo lake la ardhi na ni milima isiokuwa na uwezo wa kilimo na mifugo yeyote, lakini ni ya pili katika uchumi wa nguvu zaidi duniani Japan ni kiwanda kikubwa kipo juu ya maji, wananunua madini kutoka nje kwa ajili ya uzalishaji wa vifaa na bidhaa za viwandani na kusambaza duniani kote.

Mfano mwingine ni Uswisi, ambayo haina mashamba ya kupanda kakao (CaCao) lakini ina chocolate bora dunia nzima, Uswis ni nchi ndogo sana hairuhusu kulima kilimo au mifugo kwa zaidi ya miezi minne kwa mwaka lakini wao huzalisha maziwa bora duniani, Ni nchi ndogo lakini kwa mfano wa usalama na utaratibu wa kazi imekua nchi ya kwanza kua na hazina kuu na ya kuweka pesa katika dunia nzima kwa usalama wake.

Katika umasikini na utajiri rangi haina ushawishi. Wahamiaji au wakimbizi katika nchi za kitajiri wanaosanifiwa kua ni watu wavivu katika nchi zao ndio wamekua asili ya nguvu ya uzalishaji katika mataifa tajiri ya Ulaya.

Nini tofauti, basi?
Tofauti inakua katika tabia na kiimarishaji cha elimu na utamaduni katika miaka ya mbele.

Baada ya kuchunguza tabia za watu katika nchi zilizoendelea, tunaona kwamba wengi kufuata kanuni zifuatazo katika maisha yao:

1. Maadili. Kama kanuni ya msingi.
2. Uadilifu.
3. Jukumu.
4. Heshima kwa sheria na utaratibu.
5. Heshima ya haki za raia wengine.
6. Upendo wa kazi.
7. Kupenda uwekezaji na akiba.

Katika nchi maskini hazifati kanuni hizi, ni wachache tu ya watu katika maisha yao ya kila siku, Sisi si maskini kwa sababu ya ukosefu wa rasilimali au kwa sababu ya asili kuwa kali na sisi, Sisi ni maskini kwa sababu ya kasoro katika tabia. Kwa sababu ya kukosa uwezo wetu wa kukabiliana na kuwafundisha kanuni ya msingi iliofanya kuongozwa kwa maendeleo ya jamii na utajiri.

Nchi za kiafrika zinaukubwa wa ardhi ya kuweza kulima mazao yeyote yale na madini kila aina lakini imekosekana hazina ya kanuni za msingi zifuatazo hapo juu kuendeleza nchi zao na maisha.

Ukitazama utakuta kuwa Afrika ndiyo bara maskini.

Sijui wewe msomaji wa blog hii una maoni gani kuhusu ili wazo ili kuendeleza uchumi na maisha ya nchi za kiafrika?

No comments: