3/2/11

Interview ya Wiki


Gaddaf Katika Interview na BBC


Libya Muammar Gaddafi na mhariri wa masuala ya Mashariki ya Kati wa BBC kwa kushirikiana na Christiane Amanpour kutoka nanga ya ABC na The Times.

Jeremy Brown:
"Wewe unajulikana kwamba ni kiongozi kwa miaka mingi, Kuna watu wengi katika nchi hii wanaamini kuwa kikwazo kikubwa katika mabadiliko ni wewe.."

Kadhafi:
Kinyume kabisa. Mimi nipo kwa kuwaomba na kuwasihi mabadiliko wanaotaka, na isiwepo mabadiliko amabayo hawayataki.

Kadhafi aliulizwa kisha kuhusu uamuzi wa kupiga marufuku hivi karibuni kupitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Gaddafi:
"Mwanzo kabisa si uamuzi halali kwa sababu Baraza la Usalama na Umoja wa Mataifa si mamlaka ya kutazama kadhia kama hizi na hakuna uhalali kwa kuzingatia masuala haya.

Nataka kuuliza swali:...
Mbona hawakuchukua maamuzi kama haya na hatua dhidi ya Algeria? Inajulikana vizuri kabisa kwamba jeshi la Algeria linapigana vita katika mitaa. Kila siku kule kuna hadithi.
au kwa nini hawakutumia dhidi ya Urusi wakati inapambana na Chechens? na kwa nini pia haikutumika dhidi ya Wamarekani walikuwa mapigano dhidi ya Afghanistan? Kwa nini haikutumika dhidi ya wa-Israeil ambao wanaua watu huko Gaza?

Brown:
"Jibu nini kwa hili swali?

Gaddafi:
"Kwa sababu kuna nia ya kutawala Libya." Hii inafanya watu wa Libya kudhamiria kupambana dhidi ya ukoloni-mamboleo wa nchi za "Magharibi."

" Brown: "...?
Uliridhiana katika miaka ya hivi karibuni na nchi za Magharibi. Ukakaribisha hapa Libya viongozi muhimu kama Tony Blair. Lakini sasa kuna viongozi wa nchi za Magharibi wanasema inatakiwa uondoke madarakani. Unajisikia vipi kuhusu hivyo wanavyotaka? Uliwahi kufikiria kuwa hawa ni marafiki kweli?"

Gaddafi: ".
Bila shaka, huu ni usaliti Wao hawana maadili yoyote mbali na hilo la kutaka mimi nitoke madarakani. Na kwa sababu gani mimi niache madaraka? Mimi si Mfalme au hata Raisi.!?


Brown:
"Lakini wewe ndio unawakilisha nchi yako katika Umoja wa Mataifa, na kutambuliwa na Libya pamoja na dunia nzima kuwa wewe ni Raisi wa nchi hii.

Gaddafi:
"Hiyo ni heshima kwangu, haina uhusiano na kutumia madaraka. Uingereza nani anamiliki madaraka? ni Queen Elizabeth au David Cameron? Wewe huwezi kuelewa seriakli ya Libya..?"

Brown:
"The tuna Mfalme au mkuu wa nchi na Waziri Mkuu Cameron amechaguliwa na wananchi. Je wewe unafikiria kufanya uchaguzi wa kuchagua waziri Mkuu?"

Gaddafi:
"Wewe ni kweli hufahamu mfumo wa mazoezi ya serikali ya hapa nchini Libya."

Brown: ".
"Mimi nafahamu mfumo wa serikali ya hapa Libya, Lakini wewe unajulikana kuwa ni kiongozi wa kimataifa"

Gaddafi:
"Huwezi kuelewa mfumo wa hapa. Usiseme kuwa unafahamu. na Dunia yote haifahamu mfumo a nidhamu ya wananchi wa hapa Libya. Wewe huielewi kabisa.

Brown:
"Sasa vipi wananchi wanaonyesha uwezo wa mfumo? kwa sababu baadhi ya watu ambao walitoka barabarani kufanya maandamano kuwa ni watu wako.

Gaddafi:
"Mimi sioni maandamano yoyote katika mitaa. Je wewe umeona wapi waandamanaji.?

Brown:
"Ndio mimi nimeona.

Gaddafi:
"Wapi?"

Brown:
"Mimi niliona baadhi ya maandamano katika nchi."

Gaddafi:
"Je, wao ni wafuasi wa kwetu?"

Brown: ".
"No wao si wafuasi wako Baadhia yao walikuwa hawakutaki, na wengine walikuwa na wewe.

Gaddafi: "...
"Wao si hawatutaki sisi, hamna mtu hatutaki kwa nini wasiwe na sisi? Mimi si Raisi. wao wananipenda, wananchi woote wananipenda wapo tayari kufa kwa ajili yangu.

Christiane Amanpour:
"Kama unasema wanakupenda wewe, kwa nini basi wamechukua a kutawala Benghzi na kusema wao ni dhidi yako si na wewe tena?

Gaddafi: ".
"Hao ni Al-Qaeda, si wananchi wangu, hao wamekuja kutoka nje ya nchi.."

Brown:
"Basi hao ni wale ambao wanachana mabango na picha zako na kuweka bendera ya zamani ya Mfalme?"

Gaddafi: "...
"Ni Al-Qaeda wamekwenda katika kambi za jeshi na kutawala silaha, na wao ndio wanaua wananchi na kufanya fujo, Waliopata silaha ni vijana wadogo wadogo, walianza kutupa silaha zao baada ya kuanza athari ya madawa ya kulevya waliopewa na Al-Qaeda kupotea.

Brown:
"Hao ni kama wale wanaobomoa mabango na picha zako na kuweka bendera ya Mfalme?

Gaddafi.
"Walikua ni Al-Qaeda ambao walikwenda katika kambi za jeshi na polisi wakatawala silaha na mabomu, na sasa wao ndio wanaogopesha na kuua watu na wakatoka mitaani, hawana mashitaka yeyote wala malalamiko wanachi hawana sababu ya kufanya maandamno kabisa, Katika pade zote za dunia ikiwa Libya au Nigeria au Afghanistan wao hawatoki barabarani na kufanya maandamano, wale wanaobeba silaha ni vijana vijana wadogo sana hawajui utawala na sasa wameanza kuweka chini silaha zao na kuuza na kurudi majumbani mwao, Sasa wameanza kuamka na kurudi katika akili zao za kawaida baada ya kwisha athari ya madawa ya kulevya waliopewa na Al-Qaeda."

Brown: "Kanali Gaddafi:
"Vipi utaweza kuumaliza mgogoro huu? sehemu kubwa ya nchi yako ipo chini ya udhibiti wa waasi, Kuna shinikizo kubwa kutoka umoja wa mataifa na nchi zingine juu yako kwa jinsi gani inaweza kwisha huu mgogoro?..?.

Qadhafi:
"Sisi hatupewi na tunajihadhari na shinikizo za nje."

Brown:
"Na vipi kuhusu wewe kupoteza udhibiti wa sehemu kubwa ya nchi yako?"

Qadhafi:
"Sisi tunazama wananchi wetu na wao wapo na sisi bila wasiwasi, Sisi tutabaki na wao kuanguka."

1 comment:

SIMON KITURURU said...

Kweli hii ni ya wiki , mwezi na labda mwaka!