5/23/15

MAJI NA JUISI YA LIMAO ASUBUHI NI KINGA TOSHA YA MWILI
1. Huongeza Kinga yako ya mwili hasa kupambana na magonjwa madogo kama mafua, na kikohozi kutokana na kuwa na vitamin C 2. Husafisha Mfumo wako wa chakula, kuondoa sumu mwilini na kuzuia tumbo kujaa gesi mara kwa mara 3. Huleta hewa safi kinywani. Ni Muhimu sana kwa watu wanaonuka midomo 4. Hukuongezea uchangamfu na kufanya siku yako ianze vizuri sana 5. Husaidia majeraha kupona kwa haraka kutokana na kuwa na ascorbic acid ya kutosha. Pia huimarisha mifupa 6. Husaidia mmeng’enyo wa chakula utakachokula asubuhi au mchana kwa kuondoa vikwazo vyote vinavyoweza kuzuia umeng’enyaji wa chakula. 7. Huimarisha Ngozi yako, kuondoa makunyanzi na kukupa muonekano mzuri. 8. Husaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uzito kwani maji moto ya limao huyeyusha mafuta ya kutosha. 9. Huyapa macho yako afya nzuri na kuimarisha kuona. 10. Huondoa hali ya kuhitaji kahawa kila asubuhi ambayo si nzuri kiafya.

4/1/15

KUMBUKUMBU YA SANAMU LA ASKARI

Sanamu ya Askari au Askari Monument ni sanamu iliyopo kwenye kitovu cha jiji la Daressalaam kwenye mahali ambapo mitaa ya Samora na Azikiwe (zamani: Maktaba) zinakutana. Watu wengi hawafahamu maneno yalioandikwa kwenye hili sanamu la askari huyu wa kiafrika:
Kuna maandishi ya kumbukumbu kwa Kiingereza na Kiswahili kilichoandikwa kwa herufi za Kiarabu na herufi za Kilatini pia.
Kumbukumbu kwa Kiswahili - Maandishi ya Kilatini ni kama yafuatayo:
Kumbukumbu kwa Kiswahili - Maandishi ya Kiarabu ni kama yafuatayo:
Kumbukunbu kwa Kiingereza ni kama yafuatayo:
Picha ya kumbukumbu - Askari Waafrika Mpiganoni
Picha ya kumbukumbu - Wapiganaji wa jeshi la Uingereza katika Afrika ya Mashariki (carrier corps) "Huu ni ukumbusho wa askari Waafrika wenyeji waliopigana katika Vita Kuu na ni ukumbusho pia kwa wapagazi ambao walikuwa miguu na mikono ya majeshi. Ni ukumbusho pia kwa watu wote waliotumika wakafa kwa ajili ya mfalme na nchi yao katika Afrika ya Mashariki kwenye Vita Kkuu toka mwaka 1914 mpaka 1918 . Ukipigania nchi yako ujapo umekufa watoto wako watalikumbuka jina lako."

3/27/15

HISTORIA FUPI YA SOKO KUU LA KARIAKOO

Historia ya jina Kariakoo na Soko la Kariakoo inaanzia tangu enzi za Ukoloni wa Mjerumani wakati Tanzania Bara ikiitwa Tanganyika. Mahala lilipo Soko la Kariakoo palijengwa jengo na utawala wa  Wajerumani ambalo lilikusudiwa litumike kama ukumbi wa kuadhimishwa na kutawazwa kwa Mfalme Kaiser Wilheim wa Ujerumani kwa wakati huo. Lakini mara tu baada ya jengo kukamilika, Vita kuu ya Kwanza ya Dunia ilianza na Waingereza walipouteka mjii huu wa Dar es Salaam, walilitumia jengo hilo kama kambi ya jeshi kwa askari waliojulikana kama “Carrier Corps” kwa jina la kigeni, yaani wabeba mizigo likitafsiriwa kwa Kiswahili. Jina hilo la maaskari wabeba mizigo katika Kiswahili lilitamkwa “karia-koo” na liliendelea kutumika kama jina la eneo lote linalozunguka mahala hapa lilipo jengo hili la soko la Kariakoo. Hii ndio historia ya jina la Kariakoo ambalo yamkini Watanzania wengi watakuwa hawana ufahamu nalo. Baada ya vita Kuu ya Kwanza ya Dunia  kuisha mwaka 1919 na nchi yetu kuanza kutawaliwa na Waingereza, jengo hilo lilianza kutumika kama Soko na kuhudumia wakazi a mjii huu, Wakati huo wafanyabiashara walikuwa wakiuza bidhaa zao sakafuni kwa sababu hapakuwa na meza, Wafanya biashara waliendelea kufanya  biashara sakafuni hadi miaka ya 1960 wakati meza za saruji zilipojengwa, Kwa kadri Jiji la Dar es Salaam lilivyokua na wakazi wake kuongezeka, ndivyo  Soko hilo la zamani lilivyokuwa likishindwa kumudu kutoa huduma nzuri kwa wananchi, Pamoja na kubanana katika soko hilo na biashara kufanyika katika mazingira yasiyoridhisha, pia halikuwa na ghala za kuhifadhia bidhaa, Hali hiyo iliwafanya viongozi wa Halimashauri ya Jiji kuona haja ya kuwa na soko kubwa na la kisasa kulingana na maendeleo ya Jiji na hivyo wakaanza kujadili uwezekano wa kujenga soko jipya.
Uamuzi wa kujenga Soko Kuu la Kariakoo la sasa, ulifanywa na Serikali mnamo mwaka 1970 baada ya majadiliano yaliochukua muda baina ya Serikali kuu na Halmashauri ya Jijikama wadau ili kuweza kutoa huduma bora kwa wakazi wa Jiji la dar Es Salaam, Serikali iliagiza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kujenga Soko jipya la kisasa ambalo lingechukua nafasi ya Soko la zamani lililokuwa hapa Kariakoo, Matarajio ya uamuzi huu wa serikali wa kujenga Soko jipya yalikuwa ni kuwapatia wakazi wa Jiji mahali au Soko kubwa ambalo lingetosheleza mahitaji yao kwa muda wa miaka 50 hadi 70 ijayo kuhusu mambo yote ya vyakula, yaani uuzaji jumla, mahala pa kuhifadhi vyakula na uuzaji wa rejareja, Mipango yote ilikamilika na ujenzi ulianza rasimi mwezi Machi 1971, Ramani ya jengo la Soko ilitayarishwa na mchoraji wa ramani za majengo  Injinia Mtanzania Mzalendo kabisaNdugu Beda J.Amuli ambaye anaishi hapa Jijini Dar es Salaam hadi sasa, Wajenzi waliojenga jengo la Soko ni Mwananchi Engineering and Contracting Company (MECCO) wakisaidiana na Wakandarasi wengine kadhaa kwa kazi mbalimbali zilizohita wataalam maalum, Shughuli zote za ujenzi zilikamilika mwezi Novemba 1975, na Soko lilifunguliwa rasmi kwa matumizi ya wananchi hapo tarehe 8 Desemba,1975 na Mwlimu Julius K. Nyerere,aliyekuwa  Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mpaka kukamilika, ujenzi wa Soko ulighalim jumla ya shilingi za Kitanzania 22 milioni. 
Pia machapisho yanayo lielezea soko hili kubwa la kariakoo yanaelezea kuwa Mkandarasi ndugu Beda J. Amuli kabla ya kuanza kazi yake aliagizwa na Hayati Mwl.Julius K.Nyerere wakati huo akiwa rais  wa nchi hii kuwa asafiri kwenda  Accra-Ghana na Lusaka-Zambia,huko alikwenda kujifunza Study tour kuhusu masoko yaliyokuwa tayari yamejengwa katika miji hiyo miwili na ndipo atengeneze ramani yake kwa ajili ya ujenzi wa soko hili ambalo tunaliona leo.Mkandarasi Mzalendo alifanya hivyo na hatimaye kuja kutoka na ramani hii ya jengo letu ambalo kimsingi kuna baadhi ya muonekano(Features) zipo katika masoko hayo mawili toka nchi hizo mbili; na baadhi ni za kipekee kabisa ambapo hata ukienda Lusaka -Zambia au Accra Ghana hutazikuta, Hii ndiyo sifa pekee inayolifanya Jengo hili la Soko kuu la Kariakoo kuwa la tofauti na masoko mengine katika Ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati pia. 
SOKO KUU LA KARIAKOO Soko la kariakoo lipo katikati ya eneo la Kariakoo katika kiwanja Na.32 Zone III na limezungukwa na mitaa ya Nyamwezi, Mkunguni, Sikuku na Tandamti. Soko lina majengo mawili ambayo yameunganishwa katika ghorofa ya chini ya aridhi. Majengo haya mawili pamoja na sehehem inayounganisha ya eneo lenye jumla ya mita 17,780. Jengo la kwanza linaweza kuitwa Soko Kubwa na jengo la pili Soko dogo. Soko kubwa limegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni ghorofa ya kwanza, ghorofa ya katikati na ghorofa ya chini (Basement). Soko dogo ni soko la rejareja ambalo si tofauti na masoko mengineya Jiji la Dar es Salaam.

3/18/15

KUDADADEKI..!!

Yanga ndiyo wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa, zilianza timu nne sasa wamebaki wenyewe tu baada ya timu nyingine tatu kutolewa kwenye hatua ya awali kwenye Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa Afrika. Wakiwa hawaaminiki sana,waliweza kuichapa Platinum ya Zimbabwe kwa mabao 5-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

1/31/12

National Geographic Islands: ZanzibarZanzibar is a semi-autonomous part of Tanzania, in East Africa. It comprises the Zanzibar Archipelago in the Indian Ocean, 25--50 kilometres (16--31 mi) off the coast of the mainland, and consists of numerous small islands and two large ones: Unguja (the main island, informally referred to as Zanzibar), and Pemba. Other nearby island countries and territories include Comoros and Mayotte to the south, Mauritius and RĂ©union to the far southeast, and the Seychelles Islands about 1,500 km to the east. Arab and Portuguese traders visited the region in early times, and it was controlled by Omanis in the 18th and 19th centuries. Britain established a protectorate (1890) that became an independent sultanate in December 1963 and a republic after an uprising in January 1964. In April 1964 it joined Tanganyika to form a new republic that was renamed Tanzania in October 1964. (Frommers, 2002) The capital of Zanzibar, located on the island of Unguja, is Zanzibar City, and its historic centre, known as Stone Town, is a World Heritage Site.

Zanzibar's main industries are spices, raffia, and tourism. In particular, the islands produce cloves, nutmeg, cinnamon and pepper. For this reason, the islands, together with Tanzania's Mafia Island, are sometimes called the Spice Islands (a term also associated with the Maluku Islands in Indonesia). Zanzibar's ecology is of note for being the home of the endemic Zanzibar Red Colobus Monkey and the (possibly extinct) Zanzibar Leopard.

6/21/11

Bill Warren Undersea Explorer To Find Osama Bin Laden Body


American treasure hunter launches search for Bin Laden’s body in depths of North Arabian Sea


Arabian SeaBill Warren makes his living searching for shipwrecks. But, now, the California man has decided to turn his attention to the Arabian Sea, where he will search for the body of Osama bin Laden.

Some may have thought we would never discover the Titanic, but this is an even more ambitious search. Treasure-hunter Bill Warren, of California, is reportedly launching an underwater search to find the body of former Al Qaeda leader Osama Bin Laden.
U.S. forces say they buried the former Al Qaeda leader at sea last month from the USS Carl Vinson warship in the North Arabian Sea.
But that is the only detail of the location that has been released.
The veteran explorer launched the hunt as he does not believe President Obama gave enough proof of the terrorist’s death.
He told TMZ he is using hi-tech equipment and several boats in the search, which he says will cost hundreds of thousands of dollars.

6/5/11

Amini Usiamini - Mfalme wa Nge


Saudi Man Eats 22 Live Scorpions.

Majid Al-Malki kutoka Saudi Arabia anakula nge 22 hai kwa sekunde 20 na kuingia katika kitabu cha Guinness Records na kuitwa Mfalme wa Nge kwa kuvunja World Record ya kula nge, Kila mwisho wa wiki anakwenda yeye na rafiki zake katika jangwa kutembea na kutafuta nge wa kula.

Interview na TV ya Al-Arabiya.

TV: Baada ya kula nge sasa hivi unahisi vipi tuambie utamu wake unakuaje?

Majid: Kwa wakati huu sasa hivi sihisi chochote lakini baada ya muda hivi kama siku mbili au tatu hivi ndio hisia zinanijia.

TV: Ni hisia gani zinakuijia?

Majid: Nahisi na hamu sana ya kulipa kisasi hasa kwa kula nge, Jamgwa ni maisha yangu nitupe katika jangwa na uniache nitakachopata na kukiona katika jangwa na kila, naweza kukaa katika lolote pale mwezi au miezi miwili bila wasiwasi wala kuhisi tabu.

TV: Anapenda maisha ya jangwani na anaamini akiishi katika jangwa hata kufa na njaa kwa sababu atakuta na atapata chakula kama vile wanyama na wadudu wa jangwani wa aina yeyote ile, anacheza na nge kabla ya kula bila kua na hofu na anaamini kua sumu ya nge haimuathiri binadamu katika maisha yake.

6/2/11

The Nine Lives of Osama bin Laden

They killed the guy and threw his body in the sea?

Whose bright idea was that?

Absurd.

Never in history has a man died so many times.
I assume this is the last time.


Mpaka wakati huu ni watu wengi duniani kote hawajaamini kwa kifo cha Osama bin Laden, ni kweli kauliwa na wamerikani au alikwishakufa toka zamani..!!??

4/5/11

Kipaji cha Mpira

Tanzanian Lady Plays Football.


Lady from Morogoro, Tanzania does amazing tricks with a football.
Mwanamke kutoka Morogoro, Tanzania anakipaji cha ku-control mpira vizuri sana.

What is the difference - Kuna Tofauti Gani..!!??


3/11/11

Tsunami Hits Japan After 8.9 Megaquake
Japan was struck by a magnitude-8.8 earthquake off its northeastern coast, triggering a 4-metre tsunami that washed away cars and tore away buildings along the coast near the epicentre.

An 8.9-magnitude earthquake hit northern Japan on Friday, triggering tsunamis and sending a massive wave filled with debris that included boats and houses inching toward land.

Japan was hit by a massive earthquake on Friday, which rocked buildings in Tokyo and triggered a tsunami that dashed ships onto Japan's northeast coast and sweeping cars through the streets of coastal towns.

Authorities have revised the death toll to 29. The toll is expected to go up further.

The first earthquake measuring 8.9 on the Richter Scale struck at 2.45 p.m. local time about 237 miles northeast of Tokyo at a depth of 15.2 miles, the US Geological Survey said, revising the magnitude from an earlier 7.9.

Ten nations are said to have issued tsunami-related alerts. Warnings have also been issued along the Pacific coast.