4/1/15

KUMBUKUMBU YA SANAMU LA ASKARI

Sanamu ya Askari au Askari Monument ni sanamu iliyopo kwenye kitovu cha jiji la Daressalaam kwenye mahali ambapo mitaa ya Samora na Azikiwe (zamani: Maktaba) zinakutana. Watu wengi hawafahamu maneno yalioandikwa kwenye hili sanamu la askari huyu wa kiafrika:
Kuna maandishi ya kumbukumbu kwa Kiingereza na Kiswahili kilichoandikwa kwa herufi za Kiarabu na herufi za Kilatini pia.
Kumbukumbu kwa Kiswahili - Maandishi ya Kilatini ni kama yafuatayo:
Kumbukumbu kwa Kiswahili - Maandishi ya Kiarabu ni kama yafuatayo:
Kumbukunbu kwa Kiingereza ni kama yafuatayo:
Picha ya kumbukumbu - Askari Waafrika Mpiganoni
Picha ya kumbukumbu - Wapiganaji wa jeshi la Uingereza katika Afrika ya Mashariki (carrier corps) "Huu ni ukumbusho wa askari Waafrika wenyeji waliopigana katika Vita Kuu na ni ukumbusho pia kwa wapagazi ambao walikuwa miguu na mikono ya majeshi. Ni ukumbusho pia kwa watu wote waliotumika wakafa kwa ajili ya mfalme na nchi yao katika Afrika ya Mashariki kwenye Vita Kkuu toka mwaka 1914 mpaka 1918 . Ukipigania nchi yako ujapo umekufa watoto wako watalikumbuka jina lako."

No comments: