6/5/11

Amini Usiamini - Mfalme wa Nge


Saudi Man Eats 22 Live Scorpions.

Majid Al-Malki kutoka Saudi Arabia anakula nge 22 hai kwa sekunde 20 na kuingia katika kitabu cha Guinness Records na kuitwa Mfalme wa Nge kwa kuvunja World Record ya kula nge, Kila mwisho wa wiki anakwenda yeye na rafiki zake katika jangwa kutembea na kutafuta nge wa kula.

Interview na TV ya Al-Arabiya.

TV: Baada ya kula nge sasa hivi unahisi vipi tuambie utamu wake unakuaje?

Majid: Kwa wakati huu sasa hivi sihisi chochote lakini baada ya muda hivi kama siku mbili au tatu hivi ndio hisia zinanijia.

TV: Ni hisia gani zinakuijia?

Majid: Nahisi na hamu sana ya kulipa kisasi hasa kwa kula nge, Jamgwa ni maisha yangu nitupe katika jangwa na uniache nitakachopata na kukiona katika jangwa na kila, naweza kukaa katika lolote pale mwezi au miezi miwili bila wasiwasi wala kuhisi tabu.

TV: Anapenda maisha ya jangwani na anaamini akiishi katika jangwa hata kufa na njaa kwa sababu atakuta na atapata chakula kama vile wanyama na wadudu wa jangwani wa aina yeyote ile, anacheza na nge kabla ya kula bila kua na hofu na anaamini kua sumu ya nge haimuathiri binadamu katika maisha yake.