6/6/10

BAADA YA KIMBUNGA PHET:


Picha hii inaonyesha vipi KMBUNGA kilivyokuja na kupita kuelekea Pakistani.


Ikulu ya Muscat


Hapa ni mji wa Mutrah kando ya bahari ikionekana.


Hii ni sehemu za mjini maji ya mvua yakipita kwa nguvu.


Katika maduka makubwa ya mjini yameingiliwa na maji.


Maji ya mvua yanavyoshuka kutoka milimani.


Hii pia ni sehemu ya mjini maji ya nguvu yanavyopita kuelekea baharini.


Moja ya maduka ya mjini yapo karibu na maji ya mvua.


Mashamba ya miti ya mitende yameathirika kwa upepo mkali na miti kuanguka.

Upepo wa Phet umeua 15 Oman

Upepo wa Phet umeua watu 15 na watu wawili kupotea mpaka sasa hivi hapa Oman kabla ya kuelekea Pakistan, mkubwa wa jeshi rasmi la wananchi amesema. Wa Omani 13 na wageni wawili wamekufa kwa upepo mkali, mapema jumamosi mkubwa wa jeshi la wananchi General Malik Al-Mamari kaiambia AFP kua watu wawili wageni waliokufa ni raia wa kiasia kutoka Bangladeshi na Pakistani. Pia akasema kuwa Phet ilipungua nguvu yake nakua dhaifu sana katika siku ya ijumaa kabla ya kuendelea na speed ya 120km kwa saa kuelekea Pakistani, ambapo watu wapatao 60,000 wameokolewa kutoka
pwani ya kusini na kupelekwa katika maeneo ya salama ya Oman.



Katika mwaka 2007, kimbunga Gonu hapa Oman, kiliua kati ya watu 49 na kusababisha uharibifu uliokadiriwa kuwa ni dola bilioni US 3.9 ($ A4.63 bilioni)

Kimbunga kwa sasa kimefika Pakistani na kuelekea Iran tunawaombea salama ndugu zetu huko.

No comments: